Afisa polisi mmoja nchini Kenya
amempiga risasi na kumuua rafiki yake wa kike pamoja na afisa
mwandamizi wa polisi aliyemkuta naye na kisha yeye pia kujiua kwa
kujipiga risasi jana usiku Igembe kaskazini, Kaunti ya Meru.
Msemaji wa Jeshi la Polisi Kenya,
Zipproh Mboroki amesema konstebo Joseph Kipngetich Cheruiyot, wa
kituo cha Laare alichukua kituoni bastola aina ya Ceska jana usiku
majira ya saa tano kwa ajili ya shughuli za ulinzi.
Baada ya kuchukua sialaha hiyo
alienda kwenye klabu na Hoteli ya Tenax na kumkuta rafiki yake wa
kike Kostebo Sheila Kioko akiywa pombe na Ispekta Mkuu Benson Mwadime
na kisha kuwapiga risasi na kuwauwa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni