Wapiganaji wa Boko Haram wamewauwa
watu kadhaa na kuteketeza nyumba katika uvamizi walioufanya kwenye
mji wa Borno kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Jeshi la Nigeria limesema kuwa idadi
kadhaa ya wapiganaji wa kundi hilo wakiwa kwenye magari na pikipiki
walivamia mji wa Gubio, uliopo kilomita 95 kutoka mjii mkuu wa
Maiduguri.
Mmoja wa mkazi wa mji huo
aliyekimbia machafuko, Babor Kachalla, walifanya uvamizi huo jumamosi
usiku na kuuwa watu wengi, na kuchoma moto nyumba karibu nusu mji.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni