Waziri Mkuu wa Irak Haider al-Abadi
amesema kuwa mji wa Ramadi unaweza kukombolewa kutoka mikononi mwa
Dola ya Kiislam, IS, katika siku chache.
Hata, hivyo ameviambia vyombo vya
habari kunahitajika kuungwa mkono zaidi na washirika wa Kimataifa
wanaokabiliana na IS.
Vikosi vya Irak, vimekuwa vikipata
pigo la kuzidiwa nguvu na wapiganaji wa IS kwa miaka iliyopita na
wiki iliyopita vililazimika kuachia mji wa Ramadi kwa wapiganaji
wachache wa IS.
Waziri wa Ulinzi wa Marekani jana
alisema kuwa hali hiyo inaonyesha kuwa vikosi vya Irak havina moyo wa
kupigana vita.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni