Rais Pierre Nkuruzinza wa Burundi
amekataa wito wa Umoja wa Ulaya na Marekani wa kusitisha uchaguzi
mkuu uliogubikwa na utata uliopangwa kufanyika mwezi Juni, kutokana
na hali tete ya usalama.
Akiongea na vyombo vya habari vya
magharibi, rais Nkuruzinza amesema iwapo uchaguzi mkuu hautofanywa
kama ulivyopangwa hali itazidi kuwa mbaya zaidi kuliko ilivyo hivi
sasa na kuitumbukiza nchi katika machafuko.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni