.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 12 Mei 2015

UN YASEMA PARAGUAY IMEVUNJA HAKI ZA MTOTO ALIYEBAKWA NA KUPEWA UJAUZITO

Mtaalam wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa amesema Paraguay imeshindwa kumlinda mtoto wa miaka 10 aliyebakwa, ambaye amekataliwa kutoa ujauzito.

Mtoto huyo wa kike anadaiwa kupata ujauzito huo baada ya kubakwa na baba yake wa kambo.

Mtaalamu huyo amesema uamuzi wa serikali ya Paraguay umevunja haki za mtoto huyo, na kutoa wito mtoto huyo wa kike apatiwe uangalizi wa huduma za afya.

Taifa la Paraguay limepiga marufuku utoaji wa mimba, isipokuwa pale tu ambapo maisha ya mama yapo hatarini.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni