Rais Raul Castro wa Cuba amepata
fursa ya kuongea na kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis
ambaye aliyefanikisha kurejesha hivi karibuni uhusiano baina ya Cuba
na Marekani.
Castro amemshukuru Papa Francis kwa
jitihada hizo za upatanishi, na kusema ataanza kuomba na kurejea
kanisani, iwapo Papa Francis ataendelea na jitihada zake hizo.
Kiongozi huyo wa Cuba alipitia Rome
nchini Italia, baada ya kuhudhuria maadhimisho ya ushindi wa vita
vikuu vya pili vya dunia yaliyofanyika Jijini Moscow nchini Urusi.
Kanisa Katoliki limekuwa likiendelea
na uhusiano na Cuba tangu mwaka 1959, na sasa Papa Francis
anatarajiwa kupitia Havana wakati akienda Marekani mwezi Septemba,
mwaka huu.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni