Serikali ya Irak imetoa wito wa
kutaka kuomba watu wa kujitolea kupigana na kundi la Dola ya Kiislam
(IS) ili kusaidia kuukomboa mji wa Ramadi.
Taarifa ya wizara ya imesema zoezi
la wananchi kujitolea kujiunga ni muhimu ili kuziba uhaba wa vikosi
magharibi mwa mkoa wa Anbar.
Maelfu ya watu wamekimbia Ramadi
tangu utwaliwe na kundi la Dola ya Kiislam siku ya jumapili. Wakati
huo huo Marekani inafikiria namna ya kuunga mkono vikosi vya
aridhini.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni