Utafiti unaonyesha kuwa umarufu wa
rais Uhuru Kenyatta wa Kenya umeshuka kutoka asilimia 67 kufikia
Desemba mwaka jana hadi kufikia asilimia 48 mwezi uliopita.
Matokeo ya utafiti huo uliofanywa na
kampuni ya Ipsos Ltd baina ya Machi 28 na Aprili 7, unaonyesha pia
Naibu Rais William Ruto naye umaarufu wake umeshuka kutoka asilimia
63 hadi asilimia 35 kufikia mwezi uliopita.
Kinyume chake kukubalika kwa
viongozi watatu wa muungano wa CORD Raila Odinga, Kalonzo Musyoka
pamoja na Moses Wetang’ula, kumeongezeka kiasi katika kipindi kama
hicho.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni