Watu wapatao 43, wameuwawa na
wengine 20 kujeruhiwa katika shambulio la kutumia silaha kwa watu
waliokuwa katika basi wa dhehebu la Kiislam la Shia Mjini Karachi,
nchini Pakistan.
Polisi nchini Pakistan wamesema
washambuliaji hao wa kundi lenye itikadi kali lililopigwa marufuku
waliokuwa kwenye pikipiki walilisimamisha basi hilo na kuanza
kuwafyatulia risasi abiria.
Watu wenye silaha wapatao sita
walilishambulia basi hilo lililokuwa na abiria 60, likielekea katika
eneo la ibada la Ismaili Shia kwa ajili ya kufanya ibada.
Waumini wa Kiislam wa dhehebu la
Shia ambao ni kidogo nchini Pakistan wamekuwa wakihsmbuliwa mara kwa
mara na wapiganaji waumini wa dhehebu la Sunni.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni