
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana naWaziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma Mei 11, 2015 kwa ajili ya kikao cha Bunge kinachotarajiwa kuanza Mei 12, 2015. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Chiku Galawa.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na mzee wa Kihadzabe, Mandona katika maonyesho ya wiki ya Elimu kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo Kulia ni Bibi Agnes Israel.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wanafunzi na walimu wa shule ya msingi ya Mungula ya Mkarama, Singida ambayo inawafundisha watoto wa kabila la Wahadzabe baadaya kufungua maonyesho ya wiki ya Elimu kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimsikiza mtoto wa kabila la Wahadzabe,, Kone Paschal wa darasa la kwanza katika shule ya msingi ya Bweni ya Mngulu mkoani Singida katika maonyesho ya wiki ya Elimu kwenye uwanja wa Jamhuri Dodoma leo.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipata maelezo kuhusu shughuli mbalimbali zaBritish Coucil wakati alipotembelea banda la Taasisi hiyo kwenye maonyesho ya Elimu aliyoyafungua kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni