Matumaini yameanza kupungua ya
kupata watu waliohai ndani ya meli iliyozama kwenye mto wa Yangtze
nchini China.
Meli hiyo ya The Eastern Star, ikiwa
na watu 456 wengi wao wakiwa vikongwe ilipinduka kutokana na hali
mbaya ya hewa usiku wa jumatatu.
Watu 18 wamethibitishwa kuwa
wamekufa, limesema shirika la habari la taifa na wengine 14
wameokolewa baadhi yao walikuwa wamekwama kwenye mifuko ya hewa ndani
ya meli.
Maafisa wamesema wataendelea
kuangalia manusura, lakini hii huenda ikawa ni moja ya ajali mbaya ya
majini kutokea katika miongo kadhaa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni