Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Idara
ya Oganezesheni Dr Mohamed Seif Khatibu akizungumza na Waandishi wa
Habari makao makuu Dodoma kuhushu ratiba ya kuchukua fomu leo
Wagombea Urais kupitia Chama hicho aliwataja kuwa ataanza Prof Mark
Mwandosya ,Stephen Wasira,Edward Lowasa, balozi Amina Salumu Ali na
Charles Makongoro Nyerere na Khatibu ndiye aliyepewa jukumu na Chama
hicho kutoa fomu hizo.
Wanasiasa watano wanatarajia kuchukua
fomu ya kugombea urais katika makao makuu ya chama cha Mapinduzi
(CCM) Dodoma.
Kwa mujibu wa Katibu wa Halmashauri Kuu
ya Taifa ya CCM (NEC) wa Oganaizesheni, Dk Muhammed Seif Khatib,
uchukuaji wa fomu hizo unaanza rasmi leo.
Amesema kwa mujibu wa orodha
waliyonayo, wanachama watano watachukua fomu hizo kuanzia saa nne
asubuhi hadi saa 10:30 jioni, na kila mmoja amepewa saa moja na
wametenga muda wa kuzungumza na waandishi wa habari kwa wagombea
ambao wataona inafaa kwao. Amemtaja wa kwanza kuchukua fomu kuwa ni
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu), Profesa Mark Mwandosya
kuanzia saa 4 kamili hadi saa 5:30.
Profesa Mwandosya atafuatiwa na Waziri
wa Kilimo, Chakula na Ushirika Stephen Wassira kuanzia saa 5:30 na
atafuata Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa atachukua fomu kuanzia
saa saba kamili. Wa nne atakuwa Waziri wa zamani wa Muungano, Balozi
Amina Salum Ali kuanzia saa 8:30 mchana na pazia la ufunguzi
litafungwa saa 9:30 alasiri na mtoto wa Baba wa Taifa, Mwalimu
Nyerere, Charles Makongoro Nyerere.
Baada ya kumaliza kuchukua fomu kwa
kundi la kwanza wanasiasa wengine ambao wametangaza nia ya kuwania
urais ni Lazaro Nyalandu, Frederick Sumaye, Profesa Sospeter Muhongo,
January Makamba, Mwigulu Nchemba na Luhaga Mpina.Wanaotajwa ni pamoja
Bernard Membe, William Ngeleja, Dk Titus Kamani, Luhaga Mpina,
Mizengo Pinda, Dk Asha-Rose Migiro, Shamsi Vuai Nahodha, Dk Emmanuel
Nchimbi na Dk Hamis Kigwangalla.
Katibu huyo wa Oganaizesheni amesema
uchukuaji huo wa fomu utazingatia taratibu zilizowekwa na CCM na
kutakuwa na fomu tatu zitakazopewa wagombea.Fomu ya kwanza itahusu
maelezo binafsi ya mgombea, itahusu uzoefu na ujuzi wake, nyingine
itakuwa ya kujaza orodha ya wadhamini wake na nyingine ya masharti
kama yalivyokubaliwa na Halmashauri Kuu ya Taifa.
Kwa upande wa wadhamini amesema,
mgombea atatakiwa kupata wadhamini 450 kutoka katika mikoa 15 ya
Tanzania Bara na mikoa mingine mitatu ya Tanzania Zanzibar. wagombea
hao watakapofika kuchukua fomu, wanapaswa kuwa na ada ya Sh milioni
moja na watasaini daftari maalumu kuonesha ndio waliochukua fomu.
Amewataka wagombea wengine wanaotaka
kuchukua fomu hizo kuwasiliana mapema na ofisi yao kwani alisema
wangependa kazi ya uchukuaji fomu kudumu kwa siku zisizozidi tano ili
shughuli nyingine ziendelee.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni