Mtanzania ameshinda tuzo ya ubunifu
nchini Uingereza kwa kubuni filta ya maji inayoweza kuchuja madini ya
shaba, fluoride, bakteria, virusi na kemikali za dawa za wadudu za
kunyunyuzia.
Tuzo hiyo ya ubunifu Afrika,
imetwaliwa na Mhandisi wa Kemikali Askwar Hilonga ambaye ametumia
ubunifu huo kwa kutumia teknolojia ya nano pamoja na mchanga
kusafisha maji.
Ubunifu huo wa Mtanzania Hilonga
utanufaisha asilimia 70 za kaya nchini Tanzania ambazo hazina maji
salama.
Tuzo hiyo iliyoambatana na fedha
kiasi cha paundi 25,000, ni ya kwanza kutolewa na Taasisi ya
Uingereza ya Royal Academy of Engineering.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni