Jeshi la Kenya limesema kamanda wa
kikanda wa kundi la al Shabaab la nchini Somalia ambaye pia
inasadikiwa ni raia wa Uingereza aliyejiunga na wapiganaji wa kundi
hilo, ameuwawa katika mapigano yaliyotokea mwishoni mwa wiki.
Wapiganaji 11 wa kundi hilo pamoja
na wanajeshi wawili wa Kenya walikufa baada ya kundi hilo la al
Shabaab kuvamia kambi ya jeshi la Kenya kwenye kaunti ya Lamu
kaskazini mwa mkoa wa Pwani.
Msemaji wa vikosi vya Ulinzi Kenya
Kanali David Obonyo amesema miongoni mwa waliouwawa ni Luqman Osman
Issa ambaye pia anajulikana kama Shirwa, anayetuhumiwa kuongoza
shambulio la Mpeketoni mwaka mmoja uliopita lililouwa watu 65.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni