Kundi la Al-Qaeda limethibitisha
kuwa kiongozi wao wa Penisula ya Arabia, Nasser al-Wuhayshi, ameuwawa
katika mashambulizi yaliyofanywa na ndege ya Marekani isiyo na rubani
nchini Yemen.
Kifo chake kimetangazwa na kundi la
AQAP kupitia video ya mtandaoni, ambapo pia imeeleza kwamba
wapiganaji wawili wa al-Qaeda nao wameuwawa.
Al-Wuhayshi alikuwa akionekana kuwa
ni Kamanda Mwandamizi wa pili wa al-Qaeda na aliwahi kuwa Katibu
binafsi wa kiongozi wa kundi hilo marehemu Osama Bin Laden.
Katika video hiyo pia imemtaja
mrithi wake kuwa ni mkuu wa wapiganaji wa kundi hilo Qasim al-Raymi.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni