.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 16 Juni 2015

VIONGOZI WA AFRIKA WATOA WITO WA KUPAMBANA NA VITENDO VYA UGAIDI

Viongozi wa Afrika wametoa wito wa kuboreshwa ushirikiano wa kupambana na ongezeko la mashambulizi yenye kufuata misimamo mikali ya kiimani katika maeneo tofauti ya bara hili.

Kauli hiyo ya viongozi hao wanaokutana nchini Afrika Kusini, imetolewa wakati ambapo mwana Jihad mmoja kujilipua kwa bomu na kuuwa watu 27 katika Jiji Kuu la N'Djamena nchini Chad siku ya jumatatu.

Tukio hilo linachukuliwa kuwa ni kitendo cha kulipa kisasi cha wabinagaji wa kundi la Boko Haram, kutokana na taifa la Chad kuongoza operesheni ya kijeshi ya kikanda ya kuwasambaratisha wapiganaji wa kundi hilo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni