.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 16 Juni 2015

MAWAZIRI WA MAMBO YA NDANI WA EU KUJADILI TATIZO LA WIMBI LA WAHAMIAJI

Mawaziri wa Mambo ya Ndani wa Umoja wa Ulaya watajadiliana jinsi ya kukabiliana na makumi ya maelfu ya wahamiaji wanaoingia Ulaya kila mwaka kwa kukatiza bahari ya Mediterranean.

Jambo muhimu katika mazungumzo hayo yanayofanyika Jijini Luxembourg ni kupanga namna ya kugawana wakimbizi hao kwa usawa katika mataifa yote 28 ya Umoja wa Ulaya.

Mzigo wa uhamiaji umeibua mgogoro mkubwa wa rasilimali katika mataifa ya Italia, Ugiriki na Maltese.

Hata hiyo mataifa ya kaskazini na kusini mwa Ulaya yametaka wahamiaji hao wasilazimishwe kuenda nchi wasizotaka kwenda.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni