Mwanaume wa kwanza kupandikizwa uume
duniani raia wa Afrika Kusini anatarajia kuwa baba, madaktari
waliomfanyia upasuaji wamevieleza vyombo vya habari.
Daktari Andre van der Merwe amesema
rafiki wake wa kike imeripotiwa kuwa ni mjamzito wa miezi minne, hali
inayoashiria upandikizaji huo uume kwa njia ya upasuaji umefanikiwa.
Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka
21, ambaye jina lake limehifadhiwa alipoteza uume wake wakati
alipokatwa kimakosa wakati akifanyiwa tohara.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni