Maombi yamefanyika katika taifa la
Marekani, baada ya kuuwawa kwa watu tisa katika kanisa la kihistoria
la Wamarekani wenye asili ya Afrika la Charleston, huko South
Carolina.
Mtuhumiwa wa mauaji hayo ya chuki za
kibaguzi Dylann Roof, mwenye umri wa miak 21, alikamatwa katika
kizuizi cha polisi wa barabarani huko Shelby, North Carolina.
Katika tukio hilo wanawake sita
wanaume watatu akiwemi mchungaji wa kanisa hilo walikufa, na tayari
uchunguzi wa uhalifu utokanao na chuki umeanza.
Imeelezwa kuwa kijana huyo mweupe
alipatiwa silaha aliyotumia kwa mauaji kama zawadi ya kuzaliwa.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni