Afisa kutoka Idara ya Mambo ya Nje
Zanzibar, Bi. Asiya Hamdani akitoa maelezo kuhusu majukumu
ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa
Wananchi waliokuja kutembelea Banda la Wizara lililopo katika
Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja
vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam. Kaulimbiu ya maadhimisho hayo
ni "Utumishi wa Umma katika Bara la Afrika ni Chachu ya
Kuwawezesha Wanawake, Kuongeza Ubunifu na Kuboresha Utoaji Huduma Kwa
Umma”.
Afisa matukio msaidizi kutoka Taasisi
ya APRM, Bi. Praxeda Gasper akitoa maelezo kwa mwananchi
aliyetembelea Banda la Wizara ya Mambo ya Nje.
Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje,
Bw. Thobias Tarimo naye akielezea majukumu ya Wizara ya Mambo ya Nje
kwa mmoja wa wananchi waliojitokeza kwenye maonyesho ya Wiki ya
Utumishi wa Umma kwenye Banda la Wizara hiyo.
Mkufunzi wa Chuo cha Diplomasia
kilichopo chini ya Wizara ya Mambo ya Nje, Bi. Desderia Sabuni (wa
kwanza Kushoto) naye akiwaelezea wananchi waliotembelea banda la
Wizara ya Mambo ya Nje juu ya Kozi mbalimbali zinazotolewa na Chuo
cha Diplomasia pamoja na majukumu ya Wizara kwa ujumla.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni