Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya
Burundi, imependekeza uchaguzi wa rais kuhairishwa hadi Julai 15,
baada ya maandamano ya wiki kadhaa kupinga rais Pierre Nkurunziza
kuwania urais kwa muhula wa tatu.
Tume hiyo pia inapendekeza
kucheleweshwa uchaguzi wa wabunge uliopangwa kufanyika Juni 5 hadi
Juni 26, mwaka huu.
Watu wapatao 40 wamekufa tangu
mwishoni mwa mwezi Aprili, wakati chama tawala cha Burundi
kilipomteua Nkurunziza kuwania urais kwa muhula wa tatu, na kuibua
maandamano na jaribio la mapinduzi lililoshindikana.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni