.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 29 Juni 2015

WAKUU WA IDARA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI WAMPA ZAWADI KATIBU MKUU WAO BAADA YA KUTUNIKIWA NISHANI YA UTUMISHI MREFU NA MAADILI MEMA DARAJA LA (I)

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (kulia) akimkabidhi zawadi ya Ngao ya Utumishi Mrefu na Maadili Mema, Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil, kwa niaba ya Wakuu wa Idara na Vitengo wizarani humo. Zawadi hiyo ya kushtukiza iliandaliwa na viongozi hao wa Idara baada ya hivi karibuni Rais Jakaya Kikwete kumvisha Nishani ya Utumishi Mrefu na Maadili Mema Daraja la (I), Katibu Mkuu wao katika tukio lililofanyika Ikulu, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa wizara hiyo, Lilian Mapfa. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (kulia) akimkabidhi zawadi ya ua Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil, kwa niaba ya Wakuu wa Idara na Vitengo wizarani humo. Zawadi hizo za kushtukiza ziliandaliwa na viongozi hao baada ya hivi karibuni Rais Jakaya Kikwete kumvisha Nishani ya Utumishi Mrefu na Maadili Mema Daraja la (I), Katibu Mkuu wao katika tukio lililofanyika Ikulu, jijini Dar es Salaam
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (kulia) akimkabidhi zawadi ya kitabu cha kutunzia kumbukumbu, Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil, kwa niaba ya Wakuu wa Idara na Vitengo wizarani humo. Zawadi hizo za kushtukiza ziliandaliwa na watendaji hao baada ya hivi karibuni Rais Jakaya Kikwete kumvisha Nishani ya Utumishi Mrefu na Maadili Mema Daraja la (I), Katibu Mkuu wao katika tukio lililofanyika Ikulu, jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (kushoto), akimshukuru Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa wizara hiyo, Lilian Mapfa, pamoja na Wakuu wa Idara wengine baada ya kupewa zawadi za kushtukiza na wakuu hao baada ya Katibu Mkuu huyo hivi karibuni Rais Jakaya Kikwete kumvisha Nishani ya Utumishi Mrefu na Maadili Mema Daraja la (I), katika tukio lililofanyika Ikulu, jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (kulia), akimshukuru Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani wa wizara hiyo, Martina Nguluma pamoja na Wakuu wa Idara wengine baada ya kupewa zawadi za kushtukiza na watendaji hao baada ya Katibu Mkuu huyo hivi karibuni Rais Jakaya Kikwete kumvisha Nishani ya Utumishi Mrefu na Maadili Mema Daraja la (I), katika tukio lililofanyika Ikulu, jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (kulia), akimshukuru Mkuu wa Kitengo cha Uhasibu wa wizara hiyo, Edwin Makene pamoja na Wakuu wa Idara wengine baada ya kupewa zawadi za kushtukiza na viongozi hao baada ya Katibu Mkuu huyo hivi karibuni Rais Jakaya Kikwete kumvisha Nishani ya Utumishi Mrefu na Maadili Mema Daraja la (I), katika tukio lililofanyika Ikulu, jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (wanne kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mwamini Malemi (watatu kulia), Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Lilian Mapfa (katikati), Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Haji Janabi (wanne kulia), Mkurugenzi wa Kitengo cha Manunuzi, Manyama Mapesi (watatu kushoto), Mkurugenzi wa Huduma za Sheria, Marlin Komba (kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), Jane Massawe (wapili kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Uhasibu, Edwin Makene (wapili kulia) na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Christina Mwangosi. Wakuu wa Idara wa wizara hiyo walimpa zawadi ya kushtukiza Katibu Mkuu wao baada ya hivi karibuni Rais Jakaya Kikwete kumvisha Nishani ya Utumishi Mrefu na Maadili Mema Daraja la (I).
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil akiwa amepatwa na mshangao mara baada ya kuingia Ukumbi wa Mikutano wa wizara hiyo baada ya kuona Wakuu wa Idara wa wizara yake (hawapo pichani) wakiwa wamebeba zawadi mbalimbali kwa ajili ya kumkabidhi baada ya hivi karibuni Rais Jakaya Kikwete kumvisha Nishani ya Utumishi Mrefu na Maadili Mema Daraja la (I), katika tukio lililofanyika Ikulu, jijini Dar es Salaam. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni