Baraza la chini la Congress la
nchini Chile limeridhia muswada ambao utatoafursa kwa raia wa nchi
hiyo kuweza kulima kiasi kidogo cha bangi kwa ajili ya dawa pamoja na
matumizi ya kiroho.
Muswada huo utatoa ruhusa kwa kila
raia wa Chile, kulima nyumbani miche sita ya mmea wa bangi.
Hadi sasa nchini Chile kuuza na
kusafirisha bangi ni kosa ambalo mtuhumiwa akitiwa hatiani uhukumiwa
kifungo cha zaidi ya miaka 15 jela.
Muswada huo mpya utapaswa kupitia
katika tume ya afya, na baraza la Seneti ili kuweza kuridhiwa na
kuanza kutumika rasmi.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni