Waziri katika Ofisi ya Rais Kazi
Maalum, Prof. Mark Mwandosya ametaka wabunge wote wa bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania kuhudhuria bungeni kesho ambapo rais ataingia
bungeni kulihutubia na kulivunja bunge.
Prof. Mwandosya amesema jambo la
rais kulihutubia bunge ni sula muhimu sana hivyo si vyema mbunge ama
kundi fulani la wabunge kuwepo nje ya bunge wakati rais atakapokuwa
analihutubia bunge.
Kauli hiyo ya Prof. Mwandosya
ameitoa leo Bungeni, ikiwa siku chache tu kupita tangu Mkuu wa kambi
ya Upinzani bungeni ambaye pia ni Mwenyekiti mwenza wa Umoja wa
Katika ya Wananchi (KAWA) Mhe. Freeman Mbowe kusema wabunge wa umoja
huo hawatarejea tena bungeni.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni