Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), imekanusha taarifa zilizozagaa mkoani
Dodoma za kukamatwa kwa wapambe wa mmoja wa mgombea urais kwa tiketi
ya CCM mkoani humo wakigawa rushwa.
Akiongea na waandishi
wa habari leo Mkuu wa Takukuru wa Mkoa wa Dodoma Emma Kuhanga
amesema taarifa za uvumi huo zimewafikia na kuzifanyia uchunguzi wa
kina na kubaini kuwa hazina ukweli wowote.
Kuhanga amesema
Takukuru imejipanga vizuri kudhibiti vitendo vya rushwa katika
kipindi hiki cha uchaguzi na wakati mwingine wowote, na kutoa wito
kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa za rushwa ili wazishughulikie.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni