Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya
Joesph Nkaissery amesema maafisa usalama walikuwa hawana taarifa za
uwezekano wa kutokea shambulio la al-Shabaab lililouwa wachimba
kokoto 14 na kujeruhi 11 katika Mji wa Mandera.
Shambulio hilo ambalo linafana na la
Desemba mwaka jana lililouwa wachimba kokoto 36, limeibua maswali
iwapo maafisa usalama wa Kenya walijifunza jambo juu ya kuweza
kuepusha mashambulio katika ukanda ambao watu 500 wameuwawa wengi wao
wakiwa Wakristo.
Watu 13 waliokufa katika shambulio
hilo lililofanywa saa nane usiku limefanyika karibu na kambi ya
jeshi, ambapo wengi wa waliokufa wanatokea katika kaunti ya Nyeri.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni