Wakazi wa Jiji la Nairobi na
vitongoji vyake wametakiwa kutarajia usumbufu wakati wa ziara ya rais
Barack Obama wa Marekani baadae mwezi huu.
Msemaji wa Ikulu Monoah Esipisu
amesema baadhi ya barabara zitafungwa, hata hivyo shughuli za kawaida
zitaendelea katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta.
Rais Obama anatarajiwa kutua katika
uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta, akiwa na ndege yake ya Air
Force One na baadae kuelekea Gigiri kupitia barabara ya Mombasa.
Msafara wa rai Obama utahusisha gari
lake lisilopenya risasi aina ya limo lijulikanalo kama The Beast
yaani Mnyama, pamoja na gari la huduma ya kwanza la kijeshi.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni