Mji wa Ferguson unaadhimisha mwaka
mmoja tangu kuuwawa na polisi kijana Mmarekani mweusi, Michael Brown.
Katika kilele cha maadhimisho hayo
mamia ya wakazi wa mji huo waliandamana kwenye barabara za mji katika
kumuenzi kijana huyo wakiongozwa na baba wa marehemu.
Kitendo cha kuuwawa kwa kupigwa
risasi kijana huyo mwenye umri wa miaka 18 na polisi mzungu Darren
Wilson, kiliibua maandamano katika maeneo mbalimbali ya Marekani.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni