Kocha Jose Mourinho ameibwatukia
timu ya madaktari wa timu kwa kuingia dimbani bila ya kujua ukubwa wa
jeraha alilopata Eden Hazard, na kuituhumu ingeweza kuigharimu Chelsea goli la dakika za mwisho.
Kikosi cha Chelsea kilikuwa
kimebakia na wachezaji tisa wakati wa dakika za mwisho za mchezo wa
Ligi Kuu ya Uingereza baada ya Hazard kutolewa kupatiwa matibabu na
daktari wao Eva Carneiro.
Daktari huyo alikimbia mara moja
kuingia uwanjani kumtibu Hazard, hata hivyo Mourinho amesisitiza
daktari huyo alifanya uamuzi wa makosa katika. Mchezo huo uliisha kwa
sare ya Chelsea 2-2 Swansea.
Eden Hazard akigugumia maumivu
Daktari wa Chelsea Eva Carneiro akijibizana na Mourinho



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni