Kocha Arsene Wenger amepewa ruhusa
ya kuvunja rekodi ya uhamisho ya Arsenal ili kuweza kumnasa
mshambuliaji nyota wa Real Madrid, Karim Benzema.
Washika mtutu hao wa London
wanajipanga pia kuvunja rekodi ya sasa mshahara wa Mesut Ozil wa
paundi 150,00 kwa wiki, ili kumnasa Benzema.
Wenger anahaha kumnsa Benzema katika
majira ya joto, akiamini mshambuliaji huyo wa Real Madrid
atamuwezesha kuibadili Arsenal na kuifanya itwae kombe la Ligi Kuu ya
Uingereza.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni