Afisa wa ngazi ya juu wa Marekani
katika Umoja wa Mataifa (UN), Samantha Power amesema Marekani pamoja
na nchi nyingine zinafikiria kuiwekea vikwazo Burundi kwa kukiuka
haki za binadamu.
Balozi Samantha Power amesema ipo
haja ya kuwepo kwa usawa wa kisiasa ili kuhakikisha pande zote
zinazopingana kimawazo zinaendesha siasa zake bila ghasi wala kuwepo
kwa matukio ya mauaji.
Mauji ya generali wa ngazi za juu
serikalini na jaribio la kuuwawa mwanaharakati yameongeza shinikizo
la la Jumuiya ya Kimataifa kutaka kuwepo kwa majadiliano ya kisiasa
kuinusuru Burundi.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni