Kocha Jose Mourinho ametishia
kuwapunguza wachezaji nyota wake watatu ambao amewalaumu kuchangia
Chelsea kupata kipigo jana kutoka kwa Crystal Palace, kutokana na
kucheza chini ya kiwango.
Chelsea ilijikuta ikilala nyumbani
Stamford Bridge kwa mabao 2-1 dhidi ya Crystal Palace, baada ya Joel
Ward kuifungia timu yake bao la pili na la ushindi.
Kufuatia kipigo hicho Mourinho
amesema kuwa anaanza kuishiwa na uvumilivu dhidi ya wachezaji wake
wawili ama watatu kutokana na kutofanya vizuri dimbani.
Kocha Jose Mourinho akiwa kwenye pozi la kukerwa


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni