Kocha wa Manchester United Louis van
Gaal amesema haitaji kuongeza mshambuliaji ili kuimarisha safu ya
ushambuliaji licha ya jana kutoa sare tasa na Newcastle akiwa katika
dimba la nyumbani Old Trafford.
Manchester United imefunga magoli
mawili tu katika michezo yao ya ufunguzi wa Ligi Kuu ya Uingereza na
mshambuliaji wake Wayne Rooney hajaifungia klabu yake tangu Aprili 4.
Awali Manchester United ilikuwa
ikimtaka Pedro kabla ya mshambuliaji huyo kuamua kujiunga na Chelsea
akitokea Barcelona.
Mshambuliaji wa Manchester United Rooney akijaribu kufunga goli
Memphis Depay akimfanya kipa wa Newcastle, Krul atambae kwa chenga



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni