Mtu mmoja amekufa na wengine tisa
kujeruhiwa baada ya mlipuko kutokea kwenye mtambo wa kemikali nchini
China mashariki mwa mkoa wa Shandong.
Shirika la habari la taifa la China
la Xinhua limesema ghala katika mji wa Zibo, limelipuka na
kusababisha moto ambao miale yake mikubwa imeonekana.
Mapema mwezi huu mlipuko wa kemikaki
katika ghala moja katika mji wa Tianjin, uliuwa watu 121 na kujeruhia
mamia na wengine 54 hawajulikani walipo.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni