Wafungwa 14 wa genge moja wameuwawa
gerezani kaskazini mwa El Salvador, mamlaka za mamlaka za nchi hiyo
zimeeleza.
Maafisa wamesema miili yote ya
wafungwa hao wanaume ni wa genge hatari la Barrio 18, walibainika
katika maeneo mawili tofauti wakati wa ukaguzi kwenye gereza la
Quezaltepeque.
Vifo hivyo vinaaminika vimetokana na
ugomvi wa ndani ya genge hilo na tayari mamlaka za gereza pamoja na
polisi zimeanzisha uchunguzi.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni