Shirika la Dunia la Kupambana na
Matumizi ya Dawa Michezoni (WADA), limeshtushwa mno, baada ya tuhuma
za kuvuja kwa takwimu za matumizi ya dawa zilizopigwa marufuku
michezoni.
Gazeti ya Sunday Times na Shirika la
Utangazaji la Ujerumani la ARD/WRD wamepata nakala za matokeo ya
vipimo vya sampuli za damu 12,000, za wanamichezo 5,000.
Kwa mujibu wa gazeti la Sunday Times
ushahidi unaonyesha kunaudanganyifu usiowakawaida unaofanywa na
wanariadha wakati wa michuano mikubwa duniani.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni