.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 3 Agosti 2015

MFALME SALMAN WA SAUDI ARABIA AKATISHA MAPUMZIKO YAKE HUKO RIVIERA

Mfalme Salman wa Saudi Arabia amekatisha mapumziko yake huko Riviera nchini Ufaransa ambako ufukwe wa bahari ulilazimika kufungwa kwa usalama wake na kuamsha hasira za wananchi.

Maafisa wameeleza kuwa baada ya kukaa kwa muda wa siku nane tu badala ya wiki tatu kama alivyopanga mfalme Salman amepanda ndege kuelekea Morocco.

Zaidi ya wananchi laki moja wa Ufaransa walitia saini pingamizi la kufungwa kwa fukwe hiyo ya umma ya Vallauris kwa manufaa ya mfalme huyo pekee na familia yake.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni