Naibu Waziri wa Maji, Mh Amos Makalla ametembelea mradi mkubwa wa maji toka
ziwa Victoria na kuyapeleka miji ya Kahama, Shinyanga, Ngudu, Kishapu,
vijiji 55 na Tabora.
Ziara ya Naibu Waziri ilianzia kwenye chanzo ca maji kitongoji cha
Ihelele, kijiji cha Nyanghomango kwa kugagua chanzo, sehemu ya kutibu
maji na kusukuma maji kisha kuongea na wananchi wa kijiji cha
Nyanghomango.
Aidha alikagua mradi unaoendelea kujengwa wa kupeleka maji miji ya Mwadui, Maganzo na Kishapu.
Mradi huu mkubwa wa maji unagharimu shilingi bilioni 254 na una uwezo wa
kuzalisha maji lita milioni 120 kwa siku, lakini mpaka sasa unazalisha
maji lita milioni 80 tu kwa siku na unahudumia miji ya Kahama, Shinyanga, Ngudu ,vijiji 55 vilivyopitiwa na bomba .
Kwa mujibu wa Kaimu Mkurugenzi wa Kashwasa ambao ndiyo waendeshaji wa
mradi huu, Injinia Laurance Wasala amesema Mradi huu ni mkubwa na maji
yanatosha kufikisha maji Tabora na miji ya Mwadui, Kagongwa, Isaka, Tinde, Nzega na Igunga.
Akiwa kijiji cha Nyanghomango, Naibu Waziri wa Maji amewahakikishia
wananchi kuwa Wizara ya Maji inafanya kila linalowezekana likamilishe
mradi wa maji katika kijiji hicho ambacho ndiyo chanzo.
Kuhusu mradi wa maji kupeleka maji Kishapu, Mwadui na Maganzo,
ameridhishwa na kazi nzuri inayofanywa na Kashwasa na amehaidi wizara ya
maji itafuatilia fedha wizara ya fedha zilizopitishwa katika bajeti
zitumwe Kashwasa kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo.
Naibu Waziri wa Maji, Mh Amos Makalla akionngea na waandishi wa habari kwenye mradi wa maji Kishapu
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni