Wakulima nchini Kenya itawabidi
wasubiri miezi 18, baada ya kuondolewa zuio la matumizi ya mbengu
zilizobadilishwa vinasaba, ili waweze kununua mbegu ya mahindi
iliyobadilishwa kiini tete kwa ajili ya kilimo.
Mbengu hiyo inayotengenezwa kwa
kutumia teknolojia, inasemekana inauwezo wa kudhibiti maradhi mengi
yanayotisha uhai wa mimea kwa asilimia 13, na itasaidia kuokoa kiasi
cha fedha za Kenya shilingi bilioni 7.4 kila mwaka.
Majaribio ya kisayansi yameonyesha
kuwa mbegu hiyo inaweza kudhibiti wadudu ambao wamekuwa wakichangia
kupunguza mavuno kwa tani laki nne kila mwaka, kiasi ambacho ni sawa
na kile Kenya huagiza pindi inapokabiliwa na uhaba wa chakula.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni