Watu
11 wamekufa na wengine 20 wamejeruhiwa katika tukio la kukanyagana
kwenye hekalu mashariki mwa Jimbo la Jharkhand nchini India.
Mahujaji
walikuwa wakiadhimisha sherehe ya dini ya Hindu katika mji wa Deoghar
wakati tukio la watu kukanyagana likitokea.
Matukio
ya watu kufa kwa kukanyagana ni ya kawaida kutokea nchini India
wakati wa sherehe za kidini, ambazo huvutia uwepo wa kundi kubwa la
watu huku kukiwa na hatua chache za usalama.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni