Karibu
watu milioni moja wameathiriwa na mafuriko katika maeneo mbalimbali
nchini Myanmar tangu mwezi Juni.
Serikali
ya nchi hiyo imesema watu wapatao 100 wamekufa na hekari milioni 1.2
za mpunga zimeharibiwa na mafuriko.
Ingawa
shule zimefunguliwa katika baadhi ya maeneo, tahadhari mpya ya
mafuriko imetolewa kwa watu wanaoishi kwenye Mkoa wa Irrawaddy Delta.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni