Ametoa kauli hiyo juzi usiku
(Jumatano, Agosti 19, 2015), wakati akijibu maswali ya Watanzania
waishio Uganda katika kikao kilichofanyika hoteli ya Serena jijini
Kampala.
“Serikali tulitamani sana mchakato
huu umekamilika mwaka huu ili Watanzania waishio nje ya nchi waweze
pia kushiriki uchaguzi mkuu lakini tulipoongea na wenzetu wa NEC
(Tume ya Taifa ya Uchaguzi), ilibainika kwamba isingekuwa rahisi
kupeleka mashine za BVR nje ya nchi wakati huo huo zoezi la
uandikishaji likiwa linaendelea hapa nchini…”, alisema.
“Walisema kuna suala la
uandikishaji, likimalizika kuna suala la uhakiki wa majina ya
walioandikishwa… yote haya yanataka muda na maandalizi ya kutosha,”
aliongeza Waziri Mkuu.
Alisema Serikali bado haijakata
tamaa na yeye binafsi anaamini jambo hilo linaweza kufanyika kwenye
Uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2020 bila matatizo yoyote.
Akigusia kuhusu uandikishaji wapiga
kura nchini, Waziri Mkuu alisema lengo la awali lilikuwa ni
kuandikisha wapiga kura milioni 24 lakini kutokana na takwimu na
uzoefu uliopatikana kwenye nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa
Afrika (SADC), Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ilishauri lengo la
Serikali liwe ni kuandikisha watu milioni 22.
“Lakini kama wengi mlivyosikia,
wakati hata hawajamaliza kuandikisha wakazi wa mkoa wa Dar es Salaam,
ambao ulikuwa wa mwisho, tayari tulishavuka lengo la awali la
kuandikisha watu milioni 24,” alisema.
Alisema hilo ni jambo la kujivunia
kwa sababu tangu mwanzoni, mchakato huo ulikuwa umegubikwa na kelele
nyingi na watu walihofia kwamba kwamba zoezi hilo lisingekamilika.
“Sote ni mashuhuda, watu wamejiandikisha na sasa wanakamilisha
taratibu za uhakiki,” aliongeza.
Waziri Mkuu Pinda aliwasili nchini
Uganda Jumatano usiku kwa ziara ya siku moja akimwakilisha Rais
Jakaya Kikwete kwenye maadhimisho ya miaka 100 ya Chama cha Maskauti
cha Uganda (Uganda Scouts Association – USA). Amerejea nchini jana
usiku.
Rais Yoweri Museveni ndiye mlezi wa
chama hicho na alikuwa amemwalika Rais Kikwete kwenye maadhimisho
hayo.
(mwisho)
IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU,
MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM.
IJUMAA, AGOSTI 21, 2015.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni