Kocha wa Manchester United Lous van
Gaal amebainisha beki Luke Shaw alitiririkwa na machozi baada ya
kuvunjika mguu vibaya katika mechi ya jana usiku jambo litakalomfanya
awe nje ya uwanja kwa miezi sita.
Ulimwengu wa soko ulishutushwa pale
beki wa PSV Eindhoven, Hector Moreno kumchezea vibaya Shaw na
kupelekea avunjike mara mbili mguu wake wa kulia katika mechi ya Ligi
ya Klabu Bingwa Ulaya.
Shaw alitibiwa uwanjani kwa dakika
tisa kabla ya madaktari wa timu kuamua kumwekea hewa ya oxgeni na
kumbeba kwenye machela kwenda hospitali, ambapo sasa atarejea
Manchester leo ama kesho kwa ajili ya upasuaji.
Hector Moreno akimchezea rafu beki Luke Shaw



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni