Wizara ya Elimu Kenya, inafikiria
kuzifunga shule za umma nchini Kenya kutokana na mgomo wa walimu
unaoendelea nchini humo, Waziri wa Elimu Jacob Kaimenyi amesema.
Hata hivyo Waziri Kaimenyi amefuta
uwezekano wa kuhairishwa kwa ratiba za mitihani inayoanza mwezi ujao.
Waziri Kaimenyi amekiri kuwa idadi
kubwa ya wanafunzi katika shule za msingi na sekondari za umma
hawajafundishwa tangu kuanza kwa mgomo wa walimu Septemba mosi.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni