Timu za Manchester United na
Manchester City za Uingereza jana usiku zimeanza vibaya michuano ya
Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwa kipigo katika michezo yao ya kwanza ya
michuano hiyo.
Manchester United ikiwa ugenini
ilijikuta ikikubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa PSV Eindhoven,
licha ya mshambuliaji wao mpya Memphis Depay kuifunga goli timu yake
ya zamani katika dakika ya 41.
Luciano Narsingh akifunga goli la ushindi kwa kichwa cha kuchupa chini
Nayo Manchester City imeanza kwa
kukubali kipigo cha mabao 2-1 ikiwa nyumbani dhidi ya Juventus,
katika mchezo ambao beki wa Italia Giorgio Chiellini akijikuta
akijifunga goli la kichwa kutokana na presha kutoka kwa Vincent
Kompany.
Wachezaji wa Juventus wakishangilia goli
Naye Cristiano Ronaldo ameongoza kwa
tofauti ya magoli matatu dhidi ya Lionel Messi katika Ligi ya Klabu
Bingwa Ulaya baada ya jana usiku kufunga mabao 3 peke yake na
kuisaidia Real Madrid kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya
Shakhtar Donetsk.
Matokeo mengine ya mechi za jana ni
Paris St G 2 - 0 Malmö, VfL Wolfsburg 1 - 0 CSKA, Benfica 2 - 0 FC Astana na
Galatasaray 0 - 2 Atl Madrid.





Hakuna maoni :
Chapisha Maoni