Licha ya kutolewa katika michuano ya
Wazi ya Marekani wiki iliyopita, Serena Williams ameibuka kwa aina
yake na kung'ara baada ya kuonyesha mavazi katika shoo ya mavazi
iliyofanyika Jijini New York.
Mwanamichezo huyo mwenye vipaji
kibao akiwa jukwaani akitembea miondoko ya Cat Walk alishangiliwa na
Drake ambaye anadaiwa kuwa ni mpenzi wake mpya aliyekuwa amekaa
karibu na Anna Wintour.
Onyesho hilo pia lilihudhuriwa na
modo Gigi Hadid pamoja na Lily Aldridge nao pia walionyesha kuunga
mkono onyesho hilo la mavazi na kulifanya kupamba na mastaa kibao.
Rapa Drake akiwa na Anna Wintour wakimpongeza Serena kwa kumpigia makofi



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni