.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 11 Oktoba 2015

CARLOS SAINZ KUSHIRIKI MBIO ZA MAGARI ZA RUSSIA GRAND PRIX HII LEO

Dereva wa mbio za magari za Langlanga Carlos Sainz atashiriki mbio za magari za Russia Grand Prix hii leo, licha ya kupata jali wakati wa mazoezi.

Dereva huyo Mhispania alikimbizwa hospitali huko Sochi, baada ya kugonga uzio katika kona ya 13, akiwa katika mwendo kasi, hata hivyo aliruhusiwa kutoka hospitali jana.

Shirikisho linalosimamia michuano ya mbio za magari za Langalanga FIA, limemruhusu Sainz kushiriki mbio za magari baada ya kufanyiwa vipimo na madaktari.

Kampuni ya Toro Rosso imelifanyia matengenezo gari la Sainz jana usiku na imethibitisha kuwa dereva huyo atashiriki mbio hizo za Russia Grand Prix.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni