Wachezaji tegemeo wa Manchester
City, Sergio Aguero na David Silva wanahofiwa kukosa mchezo ligi
dhidi ya mahasimu wao jadi Manchester United pamoja na mchezo wa Ligi
ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Sevilla.
Aguero anahofiwa atakuwa nje ya
dimba kwa karibu mwezi mmoja baada ya kupasuka msuli wa kwenye paja
wakatia akiichezea timu ya taifa ya Argentina, huku Silva akiwa
ameumia enka wakati akiichezea Hispania siku ya Ijumaa.
Katika mchezo huo Aguero alimudu
kucheza hadi dakika ya 22, kabla ya kutolewa kwa machela wakati
Argentina ikikubali kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Ecuador.
David Silva akichezewa rafu iliyomsababishia kuumia enka
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni