Mahakama Kuu ya Kisii nchini Kenya
imekubali kutenganisha ndoa ya mwanamke mmoja aliyeomba kutalikiana
na mumewe, kwa sharti la kuiagiza kwanza familia yake irejeshe mahari
aliyolipiwa.
Uamuzi huo wa mahakama umetolewa kwa
mawanamke huyo Rose Kerubo Maranga, aliyefungua kesi mahakamani ya
kuomba kutengana na mumewe Gideon Magwara Nyangeso aliyeishi nae kwa
miaka nane. Baba wa mwanamke amekubali kurejesha mahari.
Baba mzazi wa Rose amekubali
kureshesha mahari ya shilingi 130,000 za Kenya, ili kumnusuru binti
yake na ndoa hiyo ambayo haina upendo na ambayo imesambaratika kiasi
ya kushindwa kurekebishwa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni