.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 9 Oktoba 2015

SAFARI ZA RAIS KENYATTA, UKARIMU NA VYAKULA VYATAFUNA BAJETI YA OFISI YA RAIS

Ofisi ya rais wa Kenya imetumia shilingi bilioni 1.4 za Kenya kati ya shilingi bilioni 6.3 za bajeti yake katika mwaka wa fedha ulioisha kwa shughuli za ukarimu, mikutano pamoja pamoja na huduma za vyakula kwa mujibu wa ripoti ya Mkaguzi wa Bajeti.

Idara hiyo ya ofisi ya rais ilikuwa wakati huo ikisimamia ofisi ya rais na naibu rais, ambapo kwa pamoja zimetumia shilingi bilioni 4.3 za Kenya kwa shughuli za ukarimu, mikutano pamoja pamoja na huduma za vyakula.

Ripoti hiyo pia imebainisha kuwa ofisi ya rais imetumia shilingi milioni 203 kwa safari za nje ya nchi.

Rais Uhuru Kenyatta ambaye hajamaliza muhula wa kwanza inasemekana ameweka historia kwa kufanya safari mara mbili zaidi ya alizofanya rais aliyepita Mwai Kibaki katika mihula yake miwili ya urais.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni